Joto limekithiri hadi duniani katika mwongo uliopita: WMO

14 Disemba 2007

Shirika la UM juu ya Upimaji wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) limeripoti kwamba takwimu rasmi ilizonazo zimeonyesha muongezeko mkubwa wa hali ya joto duniani kwa kima ambacho hakijwahai kushihudiwa hapo kabla.

Kadhalika ripoti ya WMO imeonesha kuteremka sana kwa kina cha bahari ya mabarafu ya Arctic; kuongezeka kwa mafuriko haribifu, dhoruba na ukame katika sehemu nyingi za dunia mwaka huu; na pia kugunduliwa Kijishimo cha Hewa ya Ozoni katika Bahari ya Antarctic kilichosababishwa na hali ya joto liliotanda katika majira ya baridi kwenye maeneo yaliopo Kizio cha kusini ya dunia, na vile vile kumeshuhudiwa mfumko wa msimu wa hali ya hewa ya kigeugeu ya La Nina katika maeneo ya mashariki na kati ya Pasifiki ya Ikweta (Equatorial Pacific).

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter