Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano katika Mashariki ya JKK yautia wasiwasi UM

Mapigano katika Mashariki ya JKK yautia wasiwasi UM

KM wa UM Ban Ki-moon ameripoti kuingiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama na amani ya raia wanaoishi kwenye eneo la Kivu Kaskazini, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), baada ya kufumka mapigano huko yalioselelea katika siku za karibuni. Alisema KM hali hii ya vurugu inakithirisha mateso na usumbufu wa kimaisha kwa raia, kijumla.

Kadhalika, Antonio Gutteres, Kamishna Mkuu wa Shirika la Huduma za Wahamiaji (UNHCR) wiki hii ameanza ziara ya siku tano katika JKK kusailia hatua za kuchukuliwa kimataifa, haraka iwezekanavyo, kuwasaidia makumi elfu ya wahamiaji waliong’olewa makazi Kivu Kaskazini mahitaji ya kihali.