Watoto wanadai haki zao

21 Disemba 2007

Hivi majuzi, Baraza Kuu la UM lilifanyisha kikao makhsusi cha siku tatu, kilichokuwa na lengo la kufuatilia utekelezaji wa nchi wanachama wa zile ahadi zilizopendekezwa mwaka 2002 kwenye mkutano mkuu wa UM, ambapo kulipitishwa ‘mpango wa utendaji’ wa kujenga mazingira salama yatakayotunza haki na maisha bora kwa watoto wote, pote ulimwenguni. Mpango huo ulipewa muktadha usemao “Ulimwengu Unaostahili Kuishi Watoto kwa Utulivu na Amani.”

Nilibahatika kufanya mahojiano kwenye studio zetu na Millicent. Alianza kwa kujitambulisha:

"Mimi ni Millicent Oronndo Otieno, nimemaliza darasa la nane mwaka huu,niliketi kufanya mtihani wangu wa KCPE, na sasa nangojea matokeo, na nilikuwa mkubwa katika chama cha CTC, chama cha watoto, mtoto kwa mtoto, na nilikuwa mkubwa wa shule 17 Nairobi, na pia ninasaidia katika kueneza kuhusu 'Child Line Kenya' ambayoni nambari ambaye mtoto akidhibitiwa kwa namna yoyote, anapiga hiyo namba, ama kama unataka kuongeleshwa vizuri, kama unataka mawasiliano.."

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter