Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujambazi Chad mashariki wailiazimisha UM kupunguza misaada ya kiutu kwa umma muhitaji

Ujambazi Chad mashariki wailiazimisha UM kupunguza misaada ya kiutu kwa umma muhitaji

Ofisi ya UM inayohusika na Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba majambazi bado wanaendelea kuhujumu wafanyakazi wa kimataifa wanaohudumia misaada ya kiutu katika sehemu kadha nchini Chad, hali ambayo inazorotisha zile juhudi za kuitekeleza kadhia hiyo umma muhitaji.

OCHA iliripoti ya kuwa wafanyakazi wawili wa mashirika yasio ya kiserikali walishambuliwa wiki hii na maharamia kwenye mji wa N’djamena, na vile vile katika eneo la Bahai, liliopo Chad mashariki. Watumishi wa shirika la UM linalohusika na miradi ya chakula duniani, WFP, na lile linalofadhilia maendeleo ya watoto, UNICEF pamoja na mashirika mengine ya kimataifa yaliopo Chad yameamua kusita kutumia zile barabara za kienyeji kugawa misaada ya kiutu kwa wahamiaji, hususan misaada ya chakula, kwa sababu ya kukosekana usalama.