Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wachukizwa na kusikitishwa na mauaji ya Benazir Bhutto

UM wachukizwa na kusikitishwa na mauaji ya Benazir Bhutto

KM wa UM Ban Ki-moon aliripotiwa akisema kama alishtushwa na kughadhibiwa, halkadhalika, baada ya kuarifiwa kwamba kiongozi wa Chama cha PPP, na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan, Benazir Bhutto, aliuawa Alkhamisi kwa bomu la kujitolea mhanga.

Kadhalika, baada ya mashauriano rasmi ya dharura hapo Alkhamisi kwenye Baraza la Usalama, Balozi Marcello Spatafora wa Utaliana, Raisi wa Baraza kwa mwezi Disemba alisoma taarifa maalumu Baraza juu ya mauaji ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan, kwa niaba ya wajumbe wa Baraza. Alishtumu vikali “shambulio la bomu la kujitolea mhanga liliotukia katika mji wa Rawalpindi, Pakistan katika tarehe 27 Disemba 2007, liliosababisha kifo cha Benazir Bhutto pamoja na vifo na majeruhi kadha wengine.” Baraza la Usalama liliitka Serikali ya Pakistan kuonensha uvumilivu na kuimarisha utulivu pote nchini. Taarifa ya Baraza la Usalama ilisisitiza kwamba “jamii ya kimataifa imenuia kuendelea kupiga vita aina zote za ugaidi duniani, na kuahidi kwamba itayatekeleza majukumu hayo kama ilivyopendekezwa na Mkataba wa UM.”