Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapitio ya Kazi za UM 2007

Mapitio ya Kazi za UM 2007

Mnamo mwaka 2007 UM ulikabiliwa na matatizo kadha wa kadha yaliohitajia suluhu ya pamoja, kutoka jamii ya kimataifa, kwa UM kufanikiwa kulinda usalama na amani na kuimarisha maendeleo ya uchumi na jamii yatakayokuwa na natija kwa umma pote duniani.

Tatizo liliwasumbua swana walimwengu katika 2007 lilikuwa lile suala linalohusu ongezeko la hali ya joto ulimwenguni, hali ambayo ilisababisha mabadiliko makubwa ya mwendo wa majira na liliathiri sana mazingira. Kusema kweli, hali ya hewa ilikuwa haifuati dira yake ya kimaumbile na iliionekana kuwa ya kigeugeu kikubwa ambacho, baada ya utafiti mkubwa wataalamu wanaohusika na sayansi ya mazingira walithibitisha kihakika kwamba vyanzo vya maafa haya vinatokana vitendo vya wanadamu. Kwa mfano tulishuhudia katika maeneo ya ncha ya kusini ya dunia, yaani eneo la Antaktika, yale majabali na mapnde ya barafu yalioenea huko yalikuwa yakiyayuka kwa kasi kabisa kupita miaka ya kariibuni. Kadhalika, tulishuhudia ukithirishaji mkubwa duniani wa maafa ya moto uliopamba na kuenea katika sehemu nyingi za dunia. Matukio haya yaliwathibitishia wawakilishi wa kimataifa kwamba tunahitajia kujumuika na kudhibiti kipamoja athari zinazochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa katika karne ya 21, ili tunusuru maisha ya hivi sasa na kuvivua vizazi vijavyo na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa. Suala la mabadiliko ya hali ya hewa lilipewa umuhimu wa hali ya juu katika kazi za UM na mashirika yake katika mwaka 2007.

Sikiliza kwenye idhaa ya mtandao mapitio ya baadhi ya shughuli za UM katika 2007 zinazoambatana na huduma za maendeleo, ulinzi wa amani na kadhia nyengine muhimu zinzoathiri maisha ya kila siku ya umma wa kimataifa.