Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utekelezaji wa MDG katika sekta afya mkoani Tabora, Tanzania (Sehemu ya Pili)

Utekelezaji wa MDG katika sekta afya mkoani Tabora, Tanzania (Sehemu ya Pili)

Katika makala iliopita tuliripoti kwamba karibuni nilipata fursa ya kutembelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nilipokuwa huko nilizuru moja ya vijiji kumi vilivyochaguliwa rasmi na UM barani Afrika kuwa vjiji vya milenia.

Nilizuru Kijiji cha Mbola katika wilaya ya Uyui, Mkoa wa Tabora. Kijiji hiki kilichaguliwa kuwa cha mfano, kwa makusudio kwamba uzoefu utakaopatikana huko utaenezwa kwenye sehemu nyengine za taifa na, hatimaye, kuyasaidia maeneo hayo kukabiliana vyema zaidi na huduma zao za maendeleo.

Kijiji cha Mbola husaidiwa na UM pamoja na wadau wengine wa kimataifa katika utekelezaji wa miradi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs). Miradi hii huambatana na sekta mbalimbali. Kwenye ripoti iliopita tulilenga mazungumzo yetu kwenye sekta ya afya na kusailia namna sekta hiyo inavyohudumiwa Kijijini Mbola. Tulikupatieni mahojiano niliofanya na Dktr Deusdedit Mjungu, Mratibu wa Afya wa Mradi wa Kijiji cha Milenia cha Mbola ambaye alifahamisha mfumo wa mradi anaosimamia ulivyo; alielezea mafanikio yaliopatikana katika kudhibiti malaria kwenye tarafa ya Ilalongulu, na vile vile alizungumzia namna mchango wa wahisani wa kimataifa unavyotumiwa kuimarisha sekta ya afya katika Kijiji cha Mbola.

Kwenye makala hii Dktr Mjungu anaashiria mwelekeo wa utekelezaji wa Malengo ya MDGs katika Kijiji cha Mbola kabla ya mwaka 2015, kikomo ambacho jamii ya kimataifa inatarajia kupunguza kwa nusu umasikini na hali duni katika mataifa yanayoendelea.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.