Hapa na pale

2 Novemba 2007

UM, ikishirikiana na makampuni ya kimataifa ya Googles na Cisco, yenye kuongoza katika taaluma na teknolojia za ,awasiliano ya kisasa yameanzisha kipamoja anuani mpya ya mtandao itakayompatia mtumiaji kompyuta fursa ya kufuatilia, kihakika, namna miradi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) inavyotekelezwa na kuendelezwa katika maeneo mbalimbali ya dunia. ~

Baraza Kuu la UM limepitisha kwa kura 184 za upendeleo, kura nne za upinzani (ikijumuisha Marekani, Israel, Visiwa vya Marshall na Palu) azimio la kufyeka vikwazo vya biashara, kiuchumi na fedha vilivyoekewa Cuba kwa muda wa karibu nusu karne; Shirikisho la Marshall halikutia kura.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC), Bruno Cathala amewaarifu waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu ya kuwa kazi za Mahakama kwa siku za mbele zinategemea imani ya umma wa kimataifa na misaada imara ya Mataifa ambayo yatahitajika kuunga mkono kidiplomasiya shughuli zake na kuheshimu maamuzi ya Mahakama kwa kulingana na sheria za kimataifa.

[na hatimaye] Wiki hii katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa Kuzingatia Uboreshaji wa Vyoo Duniani, ambao unafanyika mjini New Delhi, India na kusimamiwa na mashirika kadha ya UM ilitilia mkazo na viongozi wa mkutano kuhusu umuhimu wa kuwepo mazingira safi na salama ya mwahali pa kufanyia haja, hususan ilivyokuwa uchafu wa mastakimu haya yamethibitika kuathiri kihali na hudhuru afya ya watu bilioni 2.6 kote ulimwenguni.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter