KM amemtuma mjumbe maalumu katika JKK kusaka amani

2 Novemba 2007

KM Ban Ki-moon ana wasiwasi mkubwa kuhusu kuendelea kwa hali ya uhasama na mapigano katika jimbo la mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK). Alisema anakhofia athari zake huenda zikafurika eneo la Maziwa Makuu na kusababisha hali ya mtafaruku na vurugu dhidi ya usalama na utulivu wa amani wa umma.

Hivi sasa KM ameamua kumpeleka Haile Menkerios, Msaidizi Maalumu juu ya Masula ya Kisiasa kuzuru mataifa ya Maziwa Makuu ili kushauriana na Serikali ya JKK na pia viongozi wengineo wa eneo hilo kuhusu taratibu za kuchukuliwa kipamoja kukomesha vurugu liliofumka huko karibuni. Mazungumzo yatalenga zaidi uwezekano wa kutafuta suluhu juu ya kiini halisi chenye kuchochea migogoro ya eneo la Maziwa Makuu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter