Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINURSO kuendeleza operesheni za amani Sahara Magharibi mpaka Aprili 2008

MINURSO kuendeleza operesheni za amani Sahara Magharibi mpaka Aprili 2008

Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuongeza muda wa operesheni za Shirika la UM la MINURSO ambazo zinatakiwa ziendelezwe hadi Aprili 2008.

Tangu 1991 Baraza la Usalama lilianzisha Shirika la MINURSO ambalo lilikabidhiwa madaraka maalumu ya kusimamia na kufuatilia kusitishwa kwa mapigano kati ya Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi, Frente Polisario na Morocco. Azimio la Baraza limeyataka makundi yote yanayohusika na suala la Sahara ya Magharibi kuonesha ujasiri na moyo wa kisiasa utakaowashinikiza kushiriki kidhati kwenye majadiliano ya kimataifa ili, hatimaye, jamii ya kimataifa iweze kuwasilisha suluhu ya kuridhisha kwa wote.