Skip to main content

Fafanuzi za Mpatanishi wa AU kwa Darfur juu ya Mkutano wa Sirte

Fafanuzi za Mpatanishi wa AU kwa Darfur juu ya Mkutano wa Sirte

Mazungumzo ya upatanishi kuhusu mgogoro wa Darfur, yaliofanyika kwenye mji wa Sirte, Libya kuanzia Oktoba 27 (2007) na kuongozwa na Mjumbe Maalumu wa KM kwa Darfur Jan Eliasson pamoja na Dktr Salim Ahmed Salim aliye Mpatanishi wa Umoja wa Afrika (AU) kwa Darfur, yamekamilisha awamu ya kwanza ya majadiliano kwa matumaini ya kuwa wadau wote watakutana tena baada ya wiki chache kusailia awamu ya pili juu ya taratibu za marekibisho zinazofaa kuchukuliwa kipamoja ili kurudisha utulivu na amani Sudan magharibi.

Mwandishi habari wa Redio ya UM, Reem Abaza alihudhuria mazungumzo ya Sirte, na alipata fursa ya kumhoji Dktr Salim Ahmed Salim, Mpatanishi wa AU kwa Darfur.

Sikiliza mazungumzo na Dktr Salim kwenye idhaa ya mtandao.