Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msanii wa Tanzania ashirikiana na UNFPA kuhudumia uzazi bora

Msanii wa Tanzania ashirikiana na UNFPA kuhudumia uzazi bora

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Muongezeko wa Watu Duniani (UNFPA)Thoraya Obaid alikumbusha kwenye risala yake ya karibuni kwamba umma wa kimataifa umeingia kwenye karne ambayo hawatovumilia tena vifo vya mama wakati wa kuzaa. Alisema UNFPA itajitahidi kufanya kila iwezalo, kwa ushirikiano na nchi husika, kuhakikisha janga hili linakomeshwa kote duniani.

Makala yetu itawasilisha mazungumzo na msanii maarufu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akielezea mchango wake na ushirikiano uliopo na UNFPA katika kuendeleza uzazi bora na salama nchini kwao.

Sikiliza mazungumzo kamili kwenye idhaa ya mtandao.