Skip to main content

Hapa na pale

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon ameihimiza Pakistan kuwatoa vizuizini wafungwa wote wapinzani waliotiwa ndani majuzi, akiwemo pia Asma Jahangir, mtaalamu anayehusika na haki za uhuru wa kidini na kiitikadi; na pia KM alipendekeza kwa wenye madaraka Pakistan kuchukua hatua za haraka kurudisha tena utawala halali wa kidemokrasia nchini.

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeashiria bei ya nafaka ulimwenguni, kwa mwaka ujao, itakuwa ya juu sana kushinda kipindi cha karibuni kwa sababu ya akiba haba ya nafaka kimataifa, ikichanganyika na matatizo ya mazao ya nafaka na kuongezeka kwa mahitaji ya nafaka hizi kimataifa, hali ambayo kijumla inazusha mfumko mkubwa wa bei za chakula ulimwenguni.

Shirika la Hifadhi ya Mazingira (UNEP) limeripoti kuanzisha miradi inayogharamiwa dola milioni 100 iliokusudiwa kuimarisha kilimo cha sukari na chai katika Afrika Mashariki kwa kutumia nishati ya nguvu ya umeme inayotumia maji, kadhia ambayo ni safi na itasaidia kupunguza tegemeo la kuagizishia mafuta ghali kutoka nje, na kukomesha tatizo la kumwagwa hewa chafu angani.

[na hatimaye] Baraza Kuu la UM limepitisha azimio la kuifanya tarehe 15 Septemba kila mwaka kuwa ni Siku ya Kimataifa kwa Demokrasia.