Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Na kwa habari za hapa na pale

Na kwa habari za hapa na pale

Mkurugenzi mkuu wa idara ya chakula duniani WFP Bi Josette Sheeran, ameonya kwamba wakazi maskini wa mashambani barani Afrika wanakabiliwa na kimbunga kikubwa cha nyongeza za bei za chakula, mabadiliko ya hali ya hewa na muengezeko wa idadi ya watu.

wajumbe wa kamati moja muhimu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa walipiga kura wiki hii kuunga mkono azimio linatotoa mwito wa kusitishwa hukumu ya kifo kote duniani, kukiwa na matumaini ya kupiga marufuku hukumu hiyo. Wajumbe 99 wakinga mkono 52 wakipinga walipitisha azimio hilo linaloeleza miongoni mwa mambo mengine kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kwamba hukumu ya kifo ni jambo linalozuia uhalifu kutendeka na kukitokea makosa ya mahakama au tatizo la kisheria ni vigumu kubadilisha hukumu ikishatekelezwa.

Shirika la wakimbizi la UM, UNHCR lilieleza wasi wasi wake mkubwa wiki hii kutokana na makumi maelfu ya watu walokua wamekimbia makazi yao na kuishi katika makambi ndani ya nchi na sasa kulazimika kukimbia tena kutokana na mapigano mepya kati ya vikosi vya serekali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na wapiganaji wa jenerali aliyeasi Laurent Nkunda huko kaskazini ya jimbo la Kivu. UNHCR inaeleza kwamba watu hao wanaokisiwa kua elfu 30 walikua wanaishi katika makambi matano, walikimbia kutokana na hofu na wala hawakushambuliwa au kuathiriwa na mapigano.