Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utumiaji wa lugha ya Kiswahili katika vyombo vya habari duniani.

Utumiaji wa lugha ya Kiswahili katika vyombo vya habari duniani.

Baraza la Kiswahili nchini Tanzania Bakita liliandaa mkutano wa pili wa vyombo vya habari duniani mjini Dar es Salaam kujadili utumiaji wa lugha hiyo na jinsi ilivyo panuka na kutumika zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 20 wakati wa mkutano wa mwisho.

Miongoni mwa mashirika ya habari ya kimataifa yailivyopeleka wawakilishi wake ni radio ya Umoja wa Mataifa, BBC radio China na radio DW. Wajumbe kutoka mashirika ya habari ya nchi za Afrika mashariki wailihudhuria pia. Abdushakur Aboud alizungumza na mwenyekiti wa BAKITA, Suleiman Hegga mjini Dar es salam na kumuliza umuhimu wa mkutano huo.