Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya watu kukimbia kwa maelfu kutoka mji mkuu wa Somalia Mogadishu kutokana na mapigano makali

Hali ya watu kukimbia kwa maelfu kutoka mji mkuu wa Somalia Mogadishu kutokana na mapigano makali

Serekali ya mpito ya Somalia inayoungwa mkono na Ethopia imefunga vituo vitatu huru vya radio wiki hii kufuatia mapigano makali kabisa mwisho mwa wiki iliyopita na kukimbia kwa karibu watu laki moja na elfu 73 kutoka Mogadishu.

Shirika la wakimbizi la UM UNHCR, linasema hali ni mbaya kabisa na kunahitajika msaada wa haraka. Abdoushakur Aboud alizungumza na msemaji wa shirika hilo mjini Nairobi Bibi Millicent Mutuli na kumuliza kwanza hali ilivyo hivi sasa kwa wakimbizi hao.