Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Kwenye majadiliano ya hadhara ya Baraza la Usalama kuzingatia hatua za kuwapatia raia wanaojikuta kwenye mazinigira ya mapigano hifadhi bora, KM Ban Ki-moon alihimza kwa Baraza kuhakikisha raia wote wanaohitajia misaada ya kihali hupatiwa misaada hiyo kidharura bila ya kuchelewa.

Tume inayosimamia Utekelezaji wa Maafikiano ya UM ya Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani (UNFCCC) imeripoti kwamba umwagaji wa hewa chafu angani, katika 2005, uliongezeka kwa kiwanngo kikubwa kabisa hali ambayo ilichochewa na harakati za viwandani katika mataifa tajiri na pia kutokana na kukuwa kwa uchumi wa mataifa wanachama wa umoja wa zamani wa Ulaya Mashariki.

[na hatimaye] Mnamo tarehe 21 Novemba (2007) UM umeanzisha rasmi Mwaka wa Kimataifa Kuimarisha Usafi, kutokana na takwimu za kimataifa zenye kuonyesha watu karibu bilioni 3 ulimwenguni, sawa na asilimia 41 ya umma wa kimataifa, bado wanaendelea kunyimwa mazingira ya usafi na salama kimaisha.