Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waalimu wa kazi za polisi wa UM wapelekwa Chad

Waalimu wa kazi za polisi wa UM wapelekwa Chad

Kundi la mwanzo la maofisa watano wa polisi kutoka Kitengo cha UM kinachohusika na Ujenzi wa Huduma za Dharura za Polisi (SPC) limepelekwa Chad wiki hii kuanzisha mafunzo maalumu ya polisi wa kuhudumia ulinzi na usalama wa wahamiaji wa ndani ya nchi 300,000 pamoja na wahamiaji wa kutoka eneo jirani la Darfur, Sudan walioathiriwa na hali ya mapigano.

Hivi sasa kuna maofisa polisi watatu wa UM (UNIPOL) katika mji mkuu wa Chad na maofisa 32 ziada watawasili huko tarehe 30 Novemba. Maofisa hawa watasaidia kuandaa mazingira halisi ya kikazi kwa polisi 300 wa UNIPOL ambao wanatazamiwa kuwasili huko baadaye kama ilivyopendekezwa na Baraza la Usalama.