Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la kusailia mazingira mapya ya utangazaji wa idhaa za Kiswahili duniani

Kongamano la kusailia mazingira mapya ya utangazaji wa idhaa za Kiswahili duniani

Hivi karibuni katika mji wa Dar es Salaam, Tanzania kulifanyika kongamano maalumu la Idhaa za Kiswahili Duniani lilioandaliwa na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA)kwa lengo la "kujenga mazingira mapya ya utangazaji."

Mimi nilipata fursa ya kuhudhuria mkutano huo ambao mijadala yake ililenga zaidi kwenye juhudi za kuwasilisha maafikiano ya pamoja yatakayosaidia kujumisha uhusiano wa karibu na idhaa za nje za Kiswahili, ikijumiisha Idhaa ya Redio ya UM.

Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria semina alikuwemo Prof Jumanne Mayoka, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha WaIslamu cha Morogoro, Tanzania. Kwenye mazungumzo niliokuwa na Profesa Mayoka nilimuuliza hii rai ya kuitisha kongamano iliohudhuriwa na watangazaji wa Kiswahili, hususan wale waliopo nchi za kigeni, hasa huleta natija za aina gani kwa wale wanaotumia Kiswahili?

Sikiliza jawabu na dokezo ya mazungumzo haya kwenye idhaa ya mtandao.