Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya ICTR yaamua hukumu iliopita iendelezwe kwa watuhumiwa watatu

Mahakama ya ICTR yaamua hukumu iliopita iendelezwe kwa watuhumiwa watatu

Korti ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) imeidhinisha kuendelzwa ile hukumu iliotolewa kabla dhidi ya watu watatu waliokuwa wakurugenzi wa vyombo vya habari Rwanda katika 1994, ambao walituhumiwa kuchochea mauaji ya halaiki dhidi ya raia wenye asili ya KiTutsi.

Nahimana na Barayagwiza waliasisia 'Radio-Television Libre des Milles Collines' nchini Rwanda. Ngeze alikuwa mhariri mkuu wa gazeti la 'Kangura.' Imethibishwa na mahakamaa ya kwamba vyombo hivi viwili vya habari vilipania kuwachochea raia WaHutu wenye siasa ziliopitwa na wakati za kihafidhina, kuwaangamiza WaTutsi na wale WaHutu wenye mtazamo wa wastani wa kisiasa.