Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi wajisalimisha kwa walinzi wa amani katika JKK

Waasi wajisalimisha kwa walinzi wa amani katika JKK

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUC) limeripoti kwamba Micho Bizaboso, kamanda wa cheo cha juu katika kundi la waasi la Jenerali Mtoro, Laurent Nkunda karibuni alijisalimisha kwa vikosi vya UM, yeye pamoja na wafuasi 14 wengine baada ya kushindwa nguvu na wanajeshi wa MONUC.

Hapo kabla waasi hawo 15 waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito nzito, walipojaribu kuuteka mnara wa simu uliopo kwenye bonde karibu na mji wa Sake, katika jimbo la Kivu Kaskazini licha ya kuonywa na vikosi vya MONUC kutoyafanya hayo. Baada ya saa chache ya mashauriano na kutambua kwamba wamezidiwa nguvu na vikosi vya MONUC waasi walikubali kusalimisha silaha zao na kupelekwa kizuzini. Waasi hawa wanatarajiwa kupatiwa mafunzo yatakayowawezesha kujiunga na Jeshi la Serikali katika siku za usoni.,