Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umechapisha kitabu cha mwongozo kusaidia vijana wa vijijini Afrika

UM umechapisha kitabu cha mwongozo kusaidia vijana wa vijijini Afrika

Mashirika mawili ya UM yanayohusika na chakula na kilimo, FAO, na miradi ya chakula duniani, WFP yamechapisha kitabu kipya cha mwongozo kuwasaidia vijana walioathiriwa na UKIMWI/VVU katika mataifa ya Afrika kusini ya Sahara kuanzisha skuli za ukulima za kuilimisha watoto mayatima ufundi na ujuzi wa ajira ya kudumu. Mafunzo haya vile vile yatwasaidia vijana wanaoishi vijijini Afrika kupata uzoefu wa kudhibiti bora akiba ya chakula kwa muda mrefu, hasa ilivyokuwa wanakabiliwa hivi sasa na mazingira magumu ya kimaisha.

Kwa mujibu wa ripoti za UM watoto mayatima milioni 40 hishi katika maeneo ya Afrika kusini ya Sahara, na kati ya fungu hilo watoto milioni 11.4 wanakadiriwa walipoteza wazee wao kutokana na UKIMWI. Mradi huu umeyalenga mataifa 11 - yakijumuisha Cameroon, Kenya, Malawi, Msumbiji, Namibia, Sudan na pia Swaziland, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.