Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMIS yalalamika watumishi wa NGOs washambuliwa kihorera Sudan

UNMIS yalalamika watumishi wa NGOs washambuliwa kihorera Sudan

Shirika la UM juu ya Amani kwa Sudan (UNMIS) limeripoti watumishi wa mashirika yasio ya kiserekali (NGOs) wanaohudumia misaada ya kiutu katika eneo hilo la vurugu bado wanaendelea kushambuliwa kihorera na makundi mbalimbali ya waasi na wahalifu wengine.

Ripoti ilitoa mfano wa tukio moja liliojiri mwanzo wa wiki ambapo maharamia wenye silaha waliteka nyara lori la shirika moja la NGO pamoja na dereva, kwenye kambi za wahamiaji za Kasab, Darfur Kaskazini, na baadaye kumwachia huru dereva. Vile vile siku hiyo hiyo watu watatu wengine wenye silaha katika mji wa El Fasher, Darfur waliteka nyara gari la UM na kutoweka.