Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za UM kuboresha huduma za maendeleo Tanzania

Juhudi za UM kuboresha huduma za maendeleo Tanzania

Kemal Dervis, Mkurugenzi Msimamizi wa Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) wiki hii alianza ziara ya siku 10 katika bara la Afrika kwa madhumuni ya kufufua tena zile juhudi za kuyakamilisha Maendeleo ya Milenia (MDGs) kwa wakati, hususan katika zile nchi ambazo bado zinazorota na kuwachwa nyuma katika kuitekeleza miradi ya kupunguza umaskini kwa nusu katika 2015.

Ziara ya safari hii Dervis ilikuwa kwenye yale mataifa yalioshiriki katika mradi ujulikanao kama “Mradi wa Huduma za UM kwa Pamoja”, na moja ya mataifa aliyoyazuru ilikuwa pia Tanzania. Tulibahatika kufanya mahojiano ya redio na Afisa wa Habari wa Ofisi ya UNDP-Dar es Salaam, Sawiche Wamunza ambaye alijaribu kuelezea madhumuni hasa ya ziara ya Mkurugenzi Msimamizi wa UNDP nchini Tanzania.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.