Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC kumtia mbaroni kiongozi wa FRPI, mtuhumiwa wa jinai ya vita DRC

ICC kumtia mbaroni kiongozi wa FRPI, mtuhumiwa wa jinai ya vita DRC

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Halaiki (ICC) imetangaza kumshika na kumweka kizuizini kwenye mji wa Hague, Uholanzi, Germain Katanga, aliyekuwa Kamanda wa kundi la wanamgambo wa FRPI (Force de Resistance Patriotique en Ituri) katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Katanga, mwenye umri wa miaka 29, ametuhumiwa kushiriki kwenye jinai ya vita na makosa yaliotengua haki za kiutu.

Katanga ametuhumiwa makosa ya jinai ya vita na kushiriki kwenye uhalifu dhidi ya utu pale katika Februari 2003 wafuasi wake walipowachinja watu karibu 200 katika kijiji cha Bogoro, na pia kuwafanya wanawake mateka kuwa kama watumwa wao wa uzinzi.