Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisa wa WFP ameachiwa huru na wenye madaraka Usomali

Ofisa wa WFP ameachiwa huru na wenye madaraka Usomali

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kutanafusi kwa kuachiwa kutoka kizuizini Idris Osman, ofisa wa shirika nchini Usomali ambaye alishikwa na kuwekwa kizuizini na wenye madaraka mjini Mogadishu kwa siku sita. Kitendo hiki kililaaniwa na KM Ban Ki-moon ambaye alikumbusha kwamba kilikiuka Mkataba wa Geneva wa 1946 juu ya Haki na Hifadhi ya Kutodhuru Watumishi wa UM.