Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano muhimu wafanyika London kuzuia vifo vya mama wazazi

Mkutano muhimu wafanyika London kuzuia vifo vya mama wazazi

Taarifa za UM zimeripoti kwamba wajumbe zaidi ya 1,800 wanaohusika na maandalizi ya sera za kitaifa, pamoja na wataalamu, wawakilishi wa mashirika yasio ya kiserekali (NGOs), wanaharakati wanaogombania haki za wanawake na vile vile watu mashuhuri kadha wa kadha kutoka nchi 100 ziada walikusanyika karibuni mjini London kwenye mkutano maalumu ulioahidi kulipa “umuhimu, wa kiwango cha juu, suala la kuboresha afya ya mama wazazi." Kadhalika wajumbe hawo waliahidi kuliingiza suala la kuboresha huduma za uzazi kwenye ajenda za miradi ya afya, kitaifa, kikanda na kimataifa.

Mwandishi habari wa Redio ya UM, Bissera Kostova alihudhuria kikao cha London na alipata fursa ya kumhoji mmoja wa wajumbe kutoka Afrika Mashariki ambaye alielezea tatizo la maradhi ya nasuri au maradhi ya fistula.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.