Skip to main content

Juhudi za kukamilisha MDGs Tabora, Tanzania

Juhudi za kukamilisha MDGs Tabora, Tanzania

Hivi karibuni nilizuru Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nilipatiwa fursa ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliohusishwa kwenye huduma za utekelezaji wa ile miradi ya UM ya inayoambatana na Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Nilizuru kijiji cha Mbola, kilichopo wilaya ya Uyui, Mkoa wa Tabora, kijiji ambacho husaidiwa na UM katika juhudi za kukabili, kwa mafanikio, ufyekaji wa umasikini na hali duni kieneo.

Tumekuandalieni vipindi kadha vya Redio ya UM vitakavyomurika huduma za maendeleo nchini Tanzania zinazoambatana na miradi ya MDGs. Makala ya awali ya mfululizo wa vipindi kuhusu utekelezaji wa Malengo ya MDGs Tanzania, inawakilisha mahojiano na Dktr Deusdedit Mjungu, Mratibu wa Afya wa Mradi wa Kijiji cha Milenia cha Mbola.

Kwa taarifa zaidi, sikiliza idhaa ya mtandao.