Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

KM amependekeza kwa Baraza la Usalama uteuzi wa kumfanya Ahmedou Ould Abdallah kuwa Mjumbe Maalumu mpya kwa Usomali, ofisa ambaye kwa sasa anaongoza Ofisi ya UM kwa Afrika Magharibi.~

Viongozi wa jamii za wenyeji wa asili waliokusanyika Makao Makuu wiki hii wametoa mwito maalumu unaoyahimiza Mataifa Wanachama kuidhinisha, wiki ijayo, katika Baraza Kuu, mwito wa UM wa kulinda na kutunza haki za kimsingi za jamii zao na kupiga marufuku ubaguzi dhidi ya wenyeji wa asili kote duniani.

UM umeanzisha kituo makhsusi cha mtandao wa internet, kutumiwa na Mataifa Wanachama kusaidia kwenye juhudi za kupunguza hewa chafu zenye kuharibu anga na mazingira ya kimataifa.

[na hatimaye] Naibu KM Asha-Rose Migiro alipohutubia wajumbe wa Kamati ya Ushauri juu ya Matumizi ya Mfuko wa Ujenzi Amani waliokusanyika Makao Makuu kwenye kikao cha awali tangu taasisi hiyo kubuniwa, alinasihi ya kwamba ni muhimu kwa Mataifa Wanachama kuimarisha mchango wao muhimu wa fedha kuyasaidia yale mataifa yanayoibuka kwenye uhasama na mapigano yasiteleze tena kwenye vurugu na machafuko.