Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inajitahidi kudhibiti homa ya Ebola katika DRC ya kati

WHO inajitahidi kudhibiti homa ya Ebola katika DRC ya kati

Shirika la Afya Duniani (WHO) wiki hii limepeleka misaada ya afya ya dharura katika jimbo la mashariki la Kasai Occidental, DRC baada ya kufumka kwa homa maututi ya Ebola katika wiki za karibuni.

Wataalamu magwiji wa afya wa kimataifa, wakichukua zana za afya na pia madawa wameshawasili katika Kasai kuhudumia wale watu waliodhurika na virusi vya homa ya Ebola. Ugonjwa wa Ebola husababisha mtu kuvuja damu kihorera na kufa haraka. WHO iliripoti ya kuwa watu 372 wanafikiriwa kuambukizwa na virusi vya Ebola na karibu 170 ya fungu hili inasemekana wameshafariki. Lakini WHO bado ilitahadharisha ya kuwa bado haijathibitisha kihakika kama wagonjwa wote walifariki kwa sababu ya Ebola au maradhi mengine, maana kuligunduliwa pia wagonjwa katika jimbo la Kasai waliopatwa na maradhi ya kuharisha damu yanayojulikana kama Shigella.