Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu lapitisha Mwito wa Kihistoria juu ya Haki za Wenyeji wa Asili

Baraza Kuu lapitisha Mwito wa Kihistoria juu ya Haki za Wenyeji wa Asili

Alkhamisi Baraza Kuu la UM limepitisha azimio la kihistoria lililoelezea haki za kimsingi kwa watu milioni 370 duniani wenye kutambuliwa kama ni wenyeji wa asili. Azimio limeharamisha ubaguzi wote dhidi ya fungu hili la kimataifa ambalo lilikuwa likitengwa kimaendeleo na nchi zao kwa muda mrefu.

KM Ban Ki-moon amepongeza kidhati mafanikio yaliopatikana kwenye Baraza Kuu ambapo idadi kubwa ya Mataifa Wanachama yamepitisha Azimio la kuheshimu Haki za Wenyeji wa Asili Duniani.