Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu ameitisha mkutano wa aina ya pekee kuimarisha maendeleo Afrika

Katibu Mkuu ameitisha mkutano wa aina ya pekee kuimarisha maendeleo Afrika

Ripoti ya mwezi Juni (2007) ya Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) ilibainisha mataifa ya Afrika yaliopo kusini ya Sahara bado yamepwelewa sana kwenye juhudi za maendeleo, kwa ujumla, na hakuna dalili haya yatafanikiwa kuyakamilisha, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ya kupunguza kwa nusu, kabla ya 2015, umasikini, njaa, maradhi na kutojua kusoma na kuandika.

Dhamira hasa ya kikao cha Tume ilikuwa ni kuzingatia na kumurika masuala yanayoambatana na malengo matatu muhimu: kwanza, kutafuta njia za kuimarisha, kimataifa, ile michango inaohitajika kuzisaidia serekali za Afrika kukamilisha kihakika sehemu tano za miradi ya MDGs – sehemu zinazoambatana na afya, ilimu, miundo mbinu, kilimo na akiba maridhawa ya chakula; pili, kulisailiwa taratibu zitakazohakikisha kuwepo utabiri unaoaminika wa misaada kutoka wafadhili, hali ambayo itaziwezesha serekali za Afrika kupanga miradi ya muda mrefu ya maendeleo, kwa kuongeza ujenzi wa mahospitali, skuli na pia kuilimisha madkatari, walimu na manasi; na tatu, kulijadiliwa namna ya kukuza ushirikiano wa natija miongoni mwa wajumbe wa Tume ya Kuongoza Utekelezaji wa MDGs katika kila taifa husika Afrika kusini ya Sahara.