Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utumizi wa musiki katika kuhamasisha watu juu ya masuala ya kijamii

Utumizi wa musiki katika kuhamasisha watu juu ya masuala ya kijamii

Mwaka 1954 Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF lilianza kuomba msaada wa watu mashuhuri hasa wasani, waimbaji na wachezaji michezo tofauti kutumia uwezo na umashuhuri wao kuhamasisha watu juu ya haki za watoto na masuala mengine yanayo husiana na watoto. Mtu wa kwanza alikua Danny Kaye aliyekua mtumbuizaji na msani mashuhiri sana aliyefariki 1987 akiwa balozi wa nia njema wa UNICEF.

Tangu wakati huo orodha imekua ndefu hadi hivi sasa mashirika yote ya Umoja wa Mataifa huwatumia watu hao mashuhuri kuendeleza na kuhamasisha watu juu ya malengo na kazi zao. Mmoja wapo wa mabalozi hao ni muimbaji kutoka Tanzania Stara Thomas, ambae mwaka huu 2007 ameteuliwa kua Balozi wa Shirika la Idadi ya Watu , UNFPA. Anasema alianza baada ya kuombwa na kundi la Utepe Mweupe, White Ribbon ya Tanzania kuwatungia nyimbo ya kuhamasisha uzazi salama.