Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za Kimataifa za kupiga marufuku mila ya kukeketwa wasichana kote duniani

Juhudi za Kimataifa za kupiga marufuku mila ya kukeketwa wasichana kote duniani

Watalamu kutoka sehemu mbali mbali za dunia pamoja na wajumbe wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, makundi ya kidini, mashirika yasiyo ya kiserekali, maafisa wa idara za usalama na wa serekali, walikutana mjini Addis Abeba mapama mwezi wa Agosti kutathmini na kujadili njia za kukomesha kabisa mila ya kukeketa wasichana.

Zaidi ya wanawake milioni 100 na wasichana kote duniani wamekeketwa kwa namna moja au nyingine wakiwa na athari za kimwili au kiakili. Akiufungua mkutano huo ulodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, UNFPA, Mkurugenzi mkazi wa shirika hilo huko Addis Abeba, Benson Morah alisisitiza jinsi ila hiyo inavyo sababisha tabia ya kikatili kuendelea katika baadhi ya maeneo duniani. Kuna nchi 16 za Kiafrika zilizopiga marufuku mila hiyo, lakini wanawake na wasichana katika mataifa 28 za Kiafrika wangali wanakabiliwa na hatari ya kukeketwa, pamoja na wengine huko Australia, Marekani na Ulaya. Bi Jane Shuma, mratibu wa mtandao wa mashirika yanayo pinga ukeketaji huko Tanzania, alihudhuria mkutano na akizungumza na Sauti ya Umoja wa Mataifa alianza kueleza juu ya mazimio yaliyopitishwa huko Addis Abeba.