Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Uhalifu na Madawa ya Kulevya Ulimwenguni (UNDOC), ikijumuika na Benki Kuu ya Dunia, wameanzisha Taratibu za kisheria Kuhakikisha Mali za Umma Zilioibiwa Zinafidiwa, kitendo kilichokusudiwa kuyasaidia mataifa masikini kurejeshewa rasilmali ya taifa iliyoibiwa na viongozi walaji rushwa, ambao walizipatia akiba hizo hifadhi kwenye vyombo vya fedha vya kigeni; fedha hizi zitakapopatikana zinatarajiwa kutumiwa kuendeleza huduma za kiuchumi na jamii zenya natija kwa taifa zima.~

Mashirika ya UM yanayohudumia miradi ya kudhibiti hatari ya mabomu yaliotegwa ardhini yamedhihirisha ripoti ya pamoja inayoonesha kupatikana mafanikio ya kutia moyo duniani kote, tangu baada ya kuidhinishwa Mkataba wa Kupiga Marufuku Mabomu ya Kutega Ardhini miaka 10 iliopita, hali ambayo imewawezesha wakulima kuzitumia tena ardhi zao kuzalisha chakula, baada ya makumi milioni ya mabomu yalipofyekwa kutoka maeneo hayo.

[na hatimaye] Tarehe 21 Septemba inaadhimishwa na UM kote duniani kuwa ni Siku ya Kimataifa Kuimarisha Amani, na KM Ban amewaomba watumishi wote wa mataifa kuiheshimu siku hii kwa kukaa kimya kwa dakika moja saa sita mchana ili kuwakumbuka wale waliojitolea mhanga kukuza amani, na pia kuukumbuka ule umma ambao bado unashiriki kwenye operesheni za amani za UM katika sehemu mbalimbali za dunia.