Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM inahitajia kufadhiliwa msaada ziada wa kijeshi kwa Darfur

UM inahitajia kufadhiliwa msaada ziada wa kijeshi kwa Darfur

Idara ya UM juu ya Operesheni za Ulinzi wa Amani Duniani (DPKO) imeripoti kutofanikiwa kufadhiliwa na nchi wanachama misaada ya vifaa na zana nzito nzito za kijeshi, pamoja na helikopta, vifaa ambavyo vinahitajika kutumiwa na vikosi mseto vya Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa, vitakavyojulikana kama vikosi vya UNAMID, vitakavyopelekwa Darfur, Sudan mwisho wa mwaka.

Kwa mujibu wa Msemaji wa KM, Michele Montas baadhi ya mataifa yalioahidi kuchangisha vikosi vya wanajeshi kusaidia ulinzi wa Darfur kuwa yameshindwa kufikia viwango viliowekwa na Umoja wa Mataifa. Hii ni moja ya sababu iliofanya Idara ya DPKO kutoa ombi la kutaka iongezewe mchango wa wanajeshi watakaotosheleza viwango vya UM.