Mkutano wa ngazi za juu kuitishwa Makao Makuu kuzingatia Darfur

23 Septemba 2007

Ijumaa, Septemba 21, kulifanyika kikao cha faragha kwenye Makao Makuu na kuhuduriwa na wawakilishi kutoka mataifa 26, ikiwemo Sudan, na pia wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama, wawakilishi wa mataifa jirani na Sudan, na wawakilishi wa Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika (AU) pamoja na maofisa wa Umoja wa Ulaya, na wawakilishi wa kutoka Umoja wa Nchi za Kiarabu, halkadhalika.

Baada ya mkutano, KM Ban alikutana na waandishi habari na alisema wajumbe waliohudhuria kikao hicho waliafikiana kuendeleza kipamoja upatanishi wa njia tatu juu ya mgogoro wa Darfur.

Sikiliza dokezo ya fafanuzi za KM Ban na Mwenyekiti wa AU Konare kwenye idhaa ya mtandao.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud