Skip to main content

Juhudi za kudumisha amani huko Burundi, suala la uhamiaji.

Juhudi za kudumisha amani huko Burundi, suala la uhamiaji.

Ni miaka miwili sasa tangu Burundi kuanza kutekeleza makubaliano ya amani, yaliyomaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu zaidi ya miaka 10 na kuharibu kabisa uchumi na maisha ya taifa hilo la Afrika ya Kati.

Katibu Mkuu msaidizi wa UM anaeshughulikia juhudi za amani alizungumza na radio ya Umoja wa Mataifa na alisema kwa ujumla Burundi imeathirika sana katika kila fani. Alisema serekali mpya ya nchi hiyo ina changamoto yenye ncha mbili. Kwanza anasema

AKMmoja ni kuendeleaza amani. Lakini pili ni kukidhi mahitaji halisi ya haki ya wananchi wanao jiondoa kutoka mapigano, hasa katika wakati huu ambapo hakuna rasilmali ya kutosha kufanya hivyo. Kwa hivyo kila kitu kimekua muhimu ikiwa ni elimu au afya, au kuwasaidia wakimbizi kurudi nyumbani au kufufua uchumi au kukabiliana vilivyo na masuala ya kisiasa

AAAnasema ni changamoto kubwa kabisa. Ni sawa na kupanda mlima wa Kilimanjaro, wakiwa mwanzo hawajanaza kupanda. Kwani anasema, inabidi waanze kufanya kila kitu kuanzia mwanzo. Anasema, sekta zote za maisha zimeathirika na vita. Jambo moja ni kwamba anasema wanasera nzuri ya kuwataka watoto wote warudi shule.

AKLakini huwezi kusema nitawandikisha watoto wote shule. Utahitaji kujenga shule mpya, utahitaji waalimu, itabidi kuwasaidia wanafunzi kufika shule. Kuna mengi ya kufanya. Kwa upande wa afya, Burundi imeathirika vibaya kwani ni sasa tu tunapo fahamu jinsi vita vilivyo haribu sana mfumo wote wa afya.

AABi McAskie anasema, kwa hakika hali ni ngumu sana na ina kua vigumu kujua ni wapi kuanza na hatua gani za kuchukuliwa. Na moja wapo ya matatizo ni kwamba nchi hiyo kwa wakati huu haina mapato yanayoingia katika hazina ya taifa, hakuna kodi zinazotozwa watu kuweza hata kutowa huduma za kawaida.

AKSababu kubwa ya hali hiyo ni kwamba, watu hawana kazi. Ni moja kati ya mataifa maskini dunianina na huwezi kukusanya kodi kutoka kwa watu wasio na mapato. Watu huko Burundi wamekua wakishi kwa kujitegemea wenyewe kwa miaka mingi, hata kabla ya vita hapaku na mapato makubwa. Kabla ya vita, watu walikua wanategemea kilimo cha kujitosheleza wenyewe.

AAAkizungumzia msaada, kamisheni mpya ya kudumisha amani yenye ushirika wa karibu na afsi ya katibu mkuu msaidizi kwa ajili ya kudumisha amani, Bi McAskie amesema tume ili buniwa ili kufuatilia mahitaji ya mataifa yanayo jaribu kudumisha amani baada ya vita, msaada ambao haukuwepo awali.

AKNa sisi tunatoa msaada wa dharura. Tunatoa huduma za kulinda amani lakini hadi pale ushirikiano wa maendeleo ya muda mrefu pamoja na jumuia ya kimataifa unaimarishwa, ni machache yanayoweza kufanyika. Na ina onekana Jumuia ya kimataifa inajiondowa pole pole. Sisi jukumu letu litakua ni kuona rasilmali inapelekwa Burundi.

AAMsaidizi Katibu Mkuu hata hivyo ana matumaini mazuri kwamba, Burundi itaweza hatimae kusimama wima na kuimarisha maendeleo yake. Anasema ana imani maovu yote yameshapita na kuna nia ya dhati ya kuleta mabadiliko katika nchi hiyo, kwani wamechukua hatua za kishujaa katika utaratibu wa amani kukabiliana na masuala magumu na wako tayari kuendelea mbele. Bi McAskie ametoa changamoto anayotowa kwa UM, Jumuia ya Kimataifa na wa-Burundi wenyewe, akisema ikiwa sote hatutaweza kuisaidia Burundi, basi nanai ataweza kuwasaidia.

AA Mapema mwezi Julai sula la uhamiaji duniani lilijadiliwa kwa mapana na marefu katika mkutano wa kimataifa juu ya uhamiaji na maendeleo mjini Brussels, Ubelgiji. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia kikao cha ufunguzi alitoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka na thabiti kutanzua matatizo makubwa yanayo wakabili wahamiaji milioni 200 duniani. Alisema tatizo hilo ni moja wapo ya changamoto kuu ya karne hii.

CutBan internationa migration is an issue ..

AAUhamiaji wa kimataifa ni suala muhimu kabisa katika karne ya 21. Vile vile ni suala gumu na lenye utata mkubwa kufahamu kwa ukamilifu kuna mengi yaliyo hatarini kuanzia haki za wahamiaji, mabilioni ya fedha kwa ajili ya uwekezaji muhimu kabisa katika maendeleo na ukuwaji wa uchumi, inabidi tufanye kazi kwa pamoja.

AAKwa upande wa Afrika, hali imezidi kua mbaya zaidi kukiwepo na mamia na mamia ya watu wakitumia boti zisizo na usalama kusafiri kutoka Senegal hadi visiwa vya Canary vinavyo tawaliwa na Hispania, au kuvuka ghuba ya Aden kutoka Somalia hadi Yemen, pamoja na wengine wanaovuka bahari ya Mediterrenean kutoka Afrika ya Kaskazini hadi Ulaya. Watu hao wote wanatoa fidia maisha yao ili kwenda kutafuta maisha bora huko Ulaya. Msemaji wa shirika la wakimbizi la UM, UNHCR, Bi Jennifer Pagonis anasema, idadi ya wanaovuka kuingia Yemen imepunguka mwaka huu lakini watu wengi zaidi wanafariki baharini.

AKKwa miezi sita ya kwanza ya mwaka huu tume orodhesha kuwasili kwa maboti 77 ya biashara ya magendo ikiwasafirisha wakimbizi, wahmiaji na wanaotafuta hifadhi elfu nane mia sita hasa kutoka Somalia na Ethopia. Na katika kipindi hicho hicho watu 367 walifariki na karibu 118 hawajulikani wako wapi. Na ni watu mia mbili na sitini walofariki na watu elfu kumi na moja mia saba walovuka ghuba kipindi hicho mwaka jana.

AABi Pagonis anasema, wahamiaji wana rubuniwa na wafanyabiashara wa magendo, makatili wasio jali maisha ya binadamu, kwa kuwalipisha fedha chungu nzima kuwavukisha na kuwatupa baharini kabla ya kuwasili pwani ya Yemen. Anasema kuna ukatili wa aina mbali mbali unaofanyika. Msemaji wa wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM, Jemini Pandya anasema shirika lake linawasaidia waafrika wengine pia wanaojaribu kufika nchi za ulaya kwa maboti ya hatari.

AKIOM inawasaidia raia 15 wa Mali ambao waliokolewa baharini wakiwa sehemu ya kundi lililo okolewa kati kati ya Mwezi wa June. Wana rudishwa nyumbani kutoka Libya. Tumewasaidia pia kundi la wa Gambia 63 ambao waliokolewa na Jeshi la majini la Moroko. Katika matukio hayo yote wahamiaji walikua wamekwama baharini kwa wiki mbili bila mafuta, chakula au maji.

AABi Pandya anasema, mataifa hayo na mengine kote duniani kwa ujumla wanaomba msaada kwa ajili ya wahamiaji wanaozidi kukwama baharini. Ana wasi wasi kwamba, msaada kwa ajili ya kazi hizo unapunguka na wanatoa mwito kwa msaada zaidi. Katibu Mkuu Ban alisitiza kwamba wana mengi ya kuchangia katika fani za uchumi, jami na utamaduni katika nchi zilizoendelea. Na kwamba daima wahamaji wamekua wakisadia familia na jami zao nyumbani, hivyo ina bidi kuchangaya nguvu hizo na kufaidika kwa kila mtu. Lakini alisema kuna hitajika mipango kabambe na ya haraka. Aliahidi msaada wa UM kupitia Mjumbe maalum kwa ajili ya uhamiaji na maendeleo, Peter Sutherland.