Ukuaji wa Idadi ya Watu huko Tanzania

3 Agosti 2007

Akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa, Christopher Mwaijonga mwakilishi mkazi msaidizi huko Tanzania, amesema kwamba, wakati wa mkutano wa Cairo juu ya Idadi ya Watu, 1994, wajumbe walisisitiza juu ya kuwekea mkazo juu ya kuwapatia uwezo wanawake kuamua wakati wanapotaka kupata mimba na kuimarisha afya ya uzazi.

Tangu wakati huo kumekuwepo na maendeleo makubwa katika fani hiyo lakini kuna kazi nyingi ya kufanya. Alisema kwa upande wa Tanzania walianzisha kampeni ya kuwataka watu kuzaa watoto wachache ili kuweza kuwangalia badala ya kuwa na wengi na kutokua na hali nzuri ya afya au kufariki kwa magonjwa. Bw. Maijonga hata hivyo alisema sera ya China ya kua na mtoto moja sio suluhisho pia kwa nchi za Afrika.

CUT: Nalijua tatizo liloko China na Ulaya ambao wanaita negative...

Huyo alikua Christhoper Mwaijonga, mwakilishi mkazi msaidizi huko Tanzania akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa kutoka Dar es Salaam. Na licha ya matumaini hayo ripoti ya Idadi ya Watu imesema kwamba karibu watu bilioni 3.3 wa dunia wataishi katika miji, wakitoka maeneo ya mashambani kutokana na sababu chungu nzima na moja wapo kuu ni umaskini na kutafuta maisha bora. Ripoti inahimiza mataifa kuchukua hatua za haraka kuweza kukabiliana na mwendendo huo hasa kwa upande wa huduma muhimu, na sera za kubuni kazi na makazi ya wanaohamia mijini.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter