Skip to main content

Hapa na pale

Hapa na pale

Mazungumzo ya utekelezaji makubaliano ya amani ya Sudan ya Kusini yanatarajiwa kuanza. Maafisa wa vyeo vya juu wa UM, watakua na duru ya kwanza ya mazungumzo na serekali ya Sudan ya Kusini kutathmini namna ya kutekeleza vizuri zaidi makubaliano ya amani ya Januari 2005 yaliyiomaliza vita vya muda mrefu huko kusini mwa nchi.

. Duru a pili ya mazungumzo yanayo simamiwa na UM juu ya mzozo wa Sahara ya Magharibi inaanza njee ya mji wa New York hii leo. Msemaji wa UM amesema kama duru ya kwanza mwezi June, mjumbe maalum wa katibu mkuu Peter van Walsum atayaongoza mazungumzo hayo ya siku mbili kati ya Morocco na Chama cha Polisario na wajumbe wan chi jirani za Algeria na Mauritania. Mwezi wa April mwaka huu baraza la usalama lilipitisha azimio kuzitaka pane zote kuanza majadiliano bila ya masharti na kwa nia njema.

. Idara ya chakula ya UM WFP imeonya wiki hii kwamba juhudi kubwa za muda mrefu za huduma za dharura na kukarabati zina hitajika kwa ajili ya mamilioni ya watu waloathirika na mafuriko kote Asia ya Kusini. Hali mbaya kabisa ya hewa kutokana na majira ya mansoon yamesababisha mafuriko huko India, Nepal na Bangladesh na kuwathiri karibu watu milioni 20. Mkurugenzi mkuu wa WFP Bi Josette Sheeran amesema baada ya maji ya mafuriko kukauka, mamilioni ya familia maskini watabaki katika hali mbaya baada ya kupoteza mazao, mifugo na hata baadhi ya familia zao.