Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM kutoa msaada kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mashirika ya UM kutoa msaada kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kiasi ya wakimbizi elfu 26 walokimbia ghasia huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaoishi Cameroon, watapokea hivi karibuni msaada walokua wanasubiri kwa muda kutoka mashirika tofauti ya UM yaliyoungana kuendesha mpango huo.

Shirika la Wakimbizi la UM, UNHCR, pamoja na mashrika mengine ya UM yalizindua wiki hii mpango wa huduma za dharura kuwasaidia wakimbizi walotawanyika kwenye mpaka wa mashariki wa Cameroon na kuishi katika hali mbali kabisa. Msemaji wa UNHCR Jennifer Pagonis alisema mjini Geneva wakati wa mkutano na waandfishi habari kwamba wakimbizi hao hasa wanawake na watoto wako katika hali mbaya kukiwepo kiasi ya asili mia 18 ya watoto wenye utapia mloo, na kiwango cha kifo cha watoto wachanga kimefikia mara sita hadi saba kiwango cha dharura katika baadhi ya maeneo.