Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miradi inayosaidiwa na UNICEF yawapatia Wa Misri maji masafi

Miradi inayosaidiwa na UNICEF yawapatia Wa Misri maji masafi

Shirika la watoto la UM, UNICEF, na taasisi ya Coca Cola barani Afrika, wameungana kuimarishwa uwezeo wa huduma za maji kwa wa Misri wa maeneo ya mashambani na mijini.

Ni vijiji vichache tu kati ya vijiji 4 500 vya Misri ambavyo vina huduma za maji masafi au mfumo wa manisipa wa kuzowa taka. Katika maeneo mengi maji masafi yanachafuliwa kutokana na kumagwa taka za nyumbani, kilimo ay viwanda katika mito ya maji. Matokeo yake ni upungufu wa maji masafi na hatimae hali mbaya ya afya ya wananchi. Naibu mwakilishi mkazi wa UNICEF huko Misri, Hannan Sulieman, amesema kuchafuliwa maji ni tatizo kubwa sana huko Misri na linalozorota kutokana na kukua kwa haraka idadi ya wakazi, pamoja na ukosefu wa akiba ya kutosha ya maji nchini humo. UNICEF imetoa dola milioni 90 kuanzisha kampeni za kuwaelimisha wananchi na mipango ya mafunzo juu ya utumiaji bora maji na kuwahamasisha watu kuhifadhi na kulinda vituo vya maji.