Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia: Mjumbe Maalum wa UM atoa mwito kwa upinzani kurudi kwenye mazungumzo

Somalia: Mjumbe Maalum wa UM atoa mwito kwa upinzani kurudi kwenye mazungumzo

Mjumbe Maalum wa katibu mkuu kwa ajili ya Somalia Francois Lonseny Fall, alitoa miwto wiki hii, kwa serekali ya mtipo ya Somalia kualika makundi ya upinzani kujiunga na mkutano wa upatanishi unaoendelea hivi sasa huko Mogadishu.

Bw Fall, akihutubia mkutano huo, amesema angelipendelea kuwaona wadau wote walolaani ghasia wakiwa ndani au njee ya nchi kushiriki katika utaratibu huo. Mjumbe maalum alitoa wito pia kwa wajumbe kujadili masuala yote ikiwa ni pamoja kugawanya madaraka na namna kuwapokonya silaha wapiganaji. Kabla ya kuhutubia mkutano huo Bw Fall, alikutana na rais Abdullahi Yusuf Ahmed na mwenye kiti wa kamati ya upatanishi Ali Mahdi Mohamed katika ikulu ya rais mjini Mogadishu. .