Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu abadili mipango ya kuwepo UM huko Chad, na Jamhuriya Afrika ya Kati

Katibu Mkuu abadili mipango ya kuwepo UM huko Chad, na Jamhuriya Afrika ya Kati

Katibu Mkuu Ban Ki-moon ametangaza mipango iliyofanyiwa marekebisho juu ya kuwepo kwa vikosi vya amani vya UM huko mashariki ya Chad na kaskazini mashariki ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako kumekuwepo na ghasia.

Amependekeza kupelekwa kwa kikosi cha Jumuia ya Ulaya na kusema UM utashughulikia kutoa mafunzo kwa polisi na masuala mengine kama haki za binadam na utawala wa sheria kwa wananchi. Mabadiliko hayo ya Bw Ban yaliyowasilishwa katika ripoti yake kwa Baraza la Usalama juu ya hali huko Chad na CAR yanatokana na kulalamika kwa serekali ya Chad ya kuwa na wasi wasi wa kuwepo kikosi cha UM nchini humo. Kaibu Mkuu hivi sasa anapendekeza kupelekwa kikosi cha EU ambacho kitachukuwa jukuma la kuwalinda wananchi na kuhakikisha msaada wa dharura unaweza kuwafikia watu na kikosi kitabaki huko kwa miezi 12.