Skip to main content

Baraza la Usalama kuongeza muda wa operesheni za AU katika Usomali

Baraza la Usalama kuongeza muda wa operesheni za AU katika Usomali

Mapema wiki hii Baraza la Usalama limepitisha, kwa kauli moja, azimio la kuongeza kwa miezi sita zaidi operesheni za ulinzi wa amani za vikosi vya AU katika Usomali. Kadhalika azimio limeunga mkono pia ile rai ya UM ya kutayarisha mswada wa ratiba ya kuanzisha operesheni za ulinzi wa amani za UM katika Usomali.