Hapa na pale

Hapa na pale

Wiki hii mjini Oslo, Norway kulifanyika mkutano maalumu, uliosaidiwa na UM, kujadilia ujuzi wa kisasa wa kutumiwa kuwasilisha Mapinduzi ya Kilimo Afrika, huduma ambayo itakuza mavuno na kuimarisha kilimo kwa umma.

[na hatimaye] Wajumbe 1,000 wanaowakilisha serekali, sekta ya biashara na viwanda na pia kuwakilisha mashirika yanayohusika na masuala ya mazingira na taasisi za utafiti, walikutana wiki hii mjini Vienna, Austria 'kuandaa ratiba ya mkutano mkuu ujao wa kimataifa utakaofanyika mwisho wa mwaka Bali, Indonesia kuzingatia udhibiti bora wa mabadiliko ya hali hewa duniani.’