Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUC yajaribu kupatanisha makundi yanayohasimiana DRC

MONUC yajaribu kupatanisha makundi yanayohasimiana DRC

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) inajishirikisha katika jukumu, lisio rasmi, la kujaribu kupatanisha vikosi vya serekali vya FARDC na wafuasi wa Jenerali aliyetoroka jeshi, Laurent Nkunda. Huduma hii inafanyika katika jimbo la kaskazini-mashariki ya nchi.

Kadhalika, MONUC imeripoti wiki hii juu ya kurejea kazini kwa watumishi wake raia wa JKK, ambao wiki iliopita waliitisha mgomo baridi kupendekeza madai yao ya kuongezwa mishahara yanakamilishwa. Mazungumzo ya kuleta suluhu ya kuridhisha juu ya masuala ya ajira na mishahara yanaendelezwa sasa hivi kati ya watumishi wazalendo na wafanyakazi wa utawala wa MONUC.