Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Afisi ya kulinda amani ya UM huko Ivory Coast imetangaza kwamba itashirikiana na uchunguzi wa kimataifa kutokan na shambulio la roketi wiki iliyopita dhidi ya ndege iliyokua ina msafirisha waziri mkuu Guillaume Soro.

. Migogoro na mapigano barani Afrika na Mashariki ya Kati ni masuali yanayotazamiwa kuchukua nafasi ya juu katika ajenda ya baraza la usalama la UM mwezi huu kufuatana na mwenyekiti wake Balozi Wang Guangya wa China. Akizungumza na waandishi habari Bw Wang alisema zaidi ya asili mia 50 ya masuala katika ajenda ya muda yanahusiana na Afrika. Vile vile alisema baadhi ya wajumbe wa baraza wameanza kuandika azimio litakalo ruhusu kuundwa kwa jeshi la pamoja la AU na UM lililopendekezwa la kulinda amani huko Darfur.

. Baraza la usalama limetoa mwito wiki hii kwa wakuu wa jamhuri ya afrika ya kati kuanzisha majadiliano na makundi ya upinzaniu na yasiyo ya kiserekali kutokana na kuongezeka wasi wasi wa kuendelea ghasia katika taifa hilo.

. Shirika la watoto la UM, UNICEF na Urafansa zimetoa msaada wenye thamani ya karibu dola laki nne ya madawa kupambana na malaria kwa Liberia katika hatua iliyo karibishwa na serekali. Waziri wa afya wa Liberia Walter Gwenigale anasema, huo ni msaada muhimu kabisa kwa wananchi, hasa wanawake na watoto, kwani anasema, kati ya watu 50 wanaokwenda hospitali kila siku 25 huwa wana malaria.