Umoja wa Mataifa kufufua utaratibu wa amani Darfur

9 Julai 2007

Mjumbe maalum wa UM aliyepewa jukumu la kufufua utaratibu wa amani katika jimbo lenye ghasia la Darfur huko Sudan amewasili Sudan wiki hii kuanza mazungumzo mepya .

Jan Eliasson mjumbe maalum wa katibu mkuu kwa ajili ya Darfur alikutana na tume ya pamoja ya upatanishi ya Jumwia ya Afrika na UM mjini Khartoum, kujadili matayarisho ya mkutano wa pamoja wa kimataifa juu ya utaratibu wa kisiasa huko Libya. Mkutano huo utakao fanyika mjini Tripoli, tarehe 15 na 16 Julai utatathmini maendeleo yaliyopatikana mnamo miezi ya hivi karibuni kuitisha mkutano wa amani kwa ajili ya Darfur ambako zaidi ya watu laki mbili wameuwawa tangu kuanza ghasia 2003. Bw Eliasson alielekea magharibi ya Darfur kwa mazungumzo na vyama vya kisiasa makundi yasiyo ya kiserekali wajumbe wa watu walokimbia makazi yao na maafisa wa jimbo wanaohusika na utaratibu wa majadiliano.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter