Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajumbe wa Afrika Magharibi wamejadili tatizo la ugaidi

Wajumbe wa Afrika Magharibi wamejadili tatizo la ugaidi

Zaidi ya darzeni moja ya nchi za Afrika magharibi zimekutana na mataifa fadhili na mashirika ya kimataifa wiki hii kujadili mahitaji ya kifundi katika kuimarisha juhudi za kupambana na ugaidi katika kana hiyo.

Afisa muandamizi wa kamati ya kupambana na ugaidi ya baraza la Usalama, Bw Sergey Karev aliwambia waandishi habari baada ya mkutano hapa New York kwamba, lengo la mkutano ni kusikia moja kwa moja juu ya mahitaji ya nchi za Afrika Magharibi na mataifa fadhili kueleza juu ya rasilmali na ujuzi walonayo katika fani hiyo.